Jumatano, 3 Desemba 2014

PATA UTANGULIZI KUHUSU PARETO NA MATUMIZI YAKE



Pareto iliingizwa na kuanza kulimwa kwa mara ya kwanza Tanzania mwaka 1931.
Zao hili la kibiashara hustawi vizuri katika Nyanda za juu za Tanzania.
Zao hili pia ni maarufu duniani kwa kuwa na maua yenye sumu aina ya kiua wadudu asili (Pyrethrins).
Sumu ya Pareto ina sifa kuu zifuatazo: Kuua wadudu kwa haraka baada ya kupata harufu yake; Inaua wadudu kwa jinsi ya pekee ikilinganishwa na sumu zinazotengenezwa viwandani;
 Haina athari kwa wanadamu katika matumizi yake; Ni rafiki wa mazingira kwa maana haiharibu mazingira ukilinganisha na zile za viwandani; Hairuhusu mdudu kujitengenezea uwezo wa kujihami.

Matumizi ya Pareto
Pareto hutumika kutengenezea madawa mbalimbali ya kuua wadudu. Makampuni ya madawa duniani hutumia sumu ya Pareto katika kutengeneza madawa,hilo ni moja.

Pili unga wa maua ya pareto hutumika kuhifadhi nafaka kama vile mahindi,maharage ili
yasishambuliwe na wadudu waharibifu.

Maoni 4 :

  1. Morogoro pareto haikubali?

    JibuFuta
  2. Kwanini zao hili halilimwi mkoani morogoro?

    JibuFuta
  3. VP processing ya pareto locally kwa lengo la kuhifadhi nafaka kwa muda mfupi ni ipi

    JibuFuta
  4. Ni vipi tunaweza kuandaa dawa ya pareto kwa kutumia malighafi za mtaani(locally preparation of pyrethrin solution)

    JibuFuta