Alhamisi, 18 Desemba 2014

JE WAIJUA MBEGU YA ZAO LA PARETO AINA YA MACHIPUKIZI?



Mbegu aina ya machipukizi hutokana na shina la zamani la pareto, shina hilo hung’olewa na baadaye huchanwa chanwa katika mche
moja moja na pasipo kuumiza mche.
 Ukisha andaa mbegu zoezi la kuandaa shamba na upandaji, linafuata. Shamba lilimwe vizuri kwa
kwa kuondoa magugu masumbufu kama Sangari. Matuta yenye sentimeta 60 toka tuta hadi tuta yaandaliwe.

Faida ya kutumia machipukizi ni
1. Mimea karibu yote hutoa maua kwa wakati mmoja
2. Ina kiwango cha juu cha sumu kwa kuwa mimea yote hufanana
3. Kipato cha maua makavu katika hekta ni kikubwa

Jumatano, 17 Desemba 2014

Je wajua namna ya kuandaa mbegu bora za Pareto?



ILI kupata Pareto bora na yenye kiwango na ubora unaotakiwa ili kukidhi mahitaji ya soko la dunia, ni  lazima kuwa na mbegu bora.
Namna ya kupata mbegu bora!
·     Chuma maua yaliyokomaa.
·     Kausha maua kwenye jua.
·     Piga maua ili kupata mbegu.
·     Pepeta ili kupata mbegu safi isiyo na pepe.
·     Andaakitalu cha mbegu na Otesha mbegu kwenye kitalu.
Mbegu huota baada ya siku 10-21, miche hukaa kitaluni kwa muda wa miezi 2-3 kisha huwa tayari kwa kupandwa.
Faida za kutumia mbegu halisi ni kwamba upatikanaji wake ni rahisi na kwamba Miche/mmea unaotokana na mbegu hizi hukua kwa nguvu sana.

Jumatano, 3 Desemba 2014

PATA UTANGULIZI KUHUSU PARETO NA MATUMIZI YAKE



Pareto iliingizwa na kuanza kulimwa kwa mara ya kwanza Tanzania mwaka 1931.
Zao hili la kibiashara hustawi vizuri katika Nyanda za juu za Tanzania.
Zao hili pia ni maarufu duniani kwa kuwa na maua yenye sumu aina ya kiua wadudu asili (Pyrethrins).
Sumu ya Pareto ina sifa kuu zifuatazo: Kuua wadudu kwa haraka baada ya kupata harufu yake; Inaua wadudu kwa jinsi ya pekee ikilinganishwa na sumu zinazotengenezwa viwandani;
 Haina athari kwa wanadamu katika matumizi yake; Ni rafiki wa mazingira kwa maana haiharibu mazingira ukilinganisha na zile za viwandani; Hairuhusu mdudu kujitengenezea uwezo wa kujihami.

Matumizi ya Pareto
Pareto hutumika kutengenezea madawa mbalimbali ya kuua wadudu. Makampuni ya madawa duniani hutumia sumu ya Pareto katika kutengeneza madawa,hilo ni moja.

Pili unga wa maua ya pareto hutumika kuhifadhi nafaka kama vile mahindi,maharage ili
yasishambuliwe na wadudu waharibifu.

KARIBU KWENYE BLOG YETU

 KARIBU KWENYE BLOG HII

Utapata taarifa mbali mbali kuhusu kilimo bora cha Pareto, nchini Tanzania.

Utajua taarifa mbali mbali za namna ya kuandaa shamba, mbegu, kutunza shamba, uvunaji na namna ya kukausha maua ya Pareto ili kuhifadhi ubora wa sumu.  

Mkurugenzi PCT Mafinga
Martine Oweka

Mahali sahihi unapoweza kuuza Pareto, popote ulipo ni kwa wakala wa PCT.

Tupo nchi nzima, inakolimwa Pareto. Wakulima waliofanikiwa kuuza zao hili PCT wamefanikiwa kiuchumi. Usisite wala kuuliza kwa jirani...uliza PCT

Wakulima wanaolima zao la Pareto watakubaliana nasi kwamba, zao hili linafaida nyingi na linaweza kumkwamua mkulima kiuchumi.
Ikiwa unaishi kwenye mikoa ambayo zao hili linastawi, anza sasa kulima Pareto, ikukwamue kiuchumi.